Waziri wa Misri aishutumu Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Misri ametupilia mbali wito kutoka Marekani wa kutaka kuongeza kasi ya kufanya mabadiliko ya kisiasa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanji Cairo

Akikataa madai ya Marekani kuondoa hali ya hatari, Ahmed Aboul Gheith amesema Marekani "isiweke" mamlaka yake katika "nchi kubwa".

Maelfu ya wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana tangu Januari 25, wakitaka rais Hosni Mubaraka kuondoka madarakani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri Geith na waziri Clinton

Maandamano hayo siku ya Jumatano yamlifika hadi katika bunge la Misri, huku ghasia na maandamano zaidi yakiripotiwa katika miji mingine.

Mkusanyiko wenye mwelekeo kwa sasa upo katika eneo la wazi la Tahrir, katikati ya jiji la Cairo, ambapo ndio kitovu cha maandamano hayo yanayoingia siku ya 17.

Haki miliki ya picha
Image caption Waandamanaji Cairo

Picha za televisheni siku ya Alhamisi zimeonesha umati ukielekea katika eneo hilo. Idadi ya watu inatarajiwa kuwa kubwa siku ya Ijumaa, baada ya waandaaji kuitisha mkusanyiko mwingine mkubwa.