Chelsea chupuchupu kwa Fulham

Chelsea wameponea chupuchupu kufungwa na Fulham, baada ya Petr Cech kuokoa mkwaju wa penati katika dakika ya 90.

Image caption Vikwazo... Torres hakuweza kufurukuta

Cech aliokoa penati iliyopigwa na Clint Dempsey, kufuatia beki mpya wa Chelsea David Luiz kumkwatua Dempsey ndani ya boksi.

Licha ya Chelsea kutawala karibu kipindi chote walishindwa katika umaliziaji, pamoja na kumtumia mshambuliaji Fernando Torres.

Chelsea inasalia katika nafasi ya tano, huku Fulham nao wakiendelea kubaki katika nafasi ya 12.