Huwezi kusikiliza tena

Sikiliza Hosni Mubarak alipojiuzulu

Katika tangazo kupitia televisheni ya taifa, makamu wa rais Omar Suleiman amesema Bw Mubarak amekabidhi madaraka kwa jeshi.

Hatua hii imekuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika mjini Cairo pamoja na miji mingine mikuu katika siku ya 18 ya maandamano ya kudai Bw Mubarak ajiuzulu.

Waandamanaji walipokea taarifa hizo kwa kushangilia, kupeperusha bendera, kukumbatiana na kupiga honi za magari. "Watu wameuangusha utawala," wamekuwa wakiimba.

Sikiliza yaliyojiri katika matangazo yetu ya DIRA YA DUNIA, wakati tukio hilo lilipotokea, ambapo wasimulzi walikuwa ni Zuhura Yunus pamoja na Peter Musembi, ambao waliungana moja kwa moja na mwandishi wa habari kutoka mjini Cairo, Ismail Mfaume, pamoja na mchambuzi anayefuatilia siasa za Misri aliyekuwa mjini Dar es Salaam, Tanzania Jenerali Ulimwengu.