Mabadiliko ya ubaguzi Afrika Kusini

Miaka miwili baada ya video kutolewa na kuwekwa kwenye mtandao wa intaneti, ikionesha wafanyakazi weusi wakidhalilishwa, Chuo Kikuu cha Free State, Afrika Kusini, kimeanza mchakato wa kubadilisha mienendo yake na kutokomeza ubaguzi wa rangi.

Hatua ya kwanza ni kuapishwa kwa Askofu Mkuu Desmond tutu, Mwafirika mweusi wa kwanza, kuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.

Image caption Desmond Tutu

Lakini hatua kubwa zaidi iliyopigwa ni kubadilisha mpangilio wa mabweni, ambao ulikuwa ukitenganisha wanafuzi weusi na wanafunzi wazungu.

Askofu Mkuu Desmond Tutu, ambaye atakumbukwa kwa ndoto zake za kuijenga Afrika Kusini kuwa taifa lisilo jali rangi na kuishi kwa umoja, ametunukiwa shahada ya heshima kutoka chuo hicho kilicho na sifa ya ubaguzi mwingi katika nchi hiyo.

Sera mbaya

Chuo hicho kimeanza mchakato wa kuwaleta watu wa rangi tofauti pamoja, itikadi ambayo Desmond Tutu mwenyewe amekuwa nayo kwa miaka mingi.

Desmond Tutu alisema 'Ni kweli kuwa sisi ni wakereketwa kutokana na sera mbaya zaidi za ukandamizaji na ndizo chanzo cha siasa za ubaguzi wa rangi.'

Image caption Desmond Tutu akiwa na Nelson Mandela

Chama tawala nchini humo, ANC, kilianzishwa katika eneo hilo la Free Sate na chama hicho kilipinga siasa za ubaguzi.

Wakati mmoja wanafunzi wazungu pekee ndio waliokubaliwa kusoma katika chuo hicho lakini kwa sasa asilimia 65 ya wanafunzi ni weusi.

Ukilinganisha na hali ilivyokuwa miaka miwili iliyopita, hii ni hatua kubwa sana.

Tabia ya kihalifu

Katika kiwanja cha chuo hicho kuna ofisi za kuwapatanisha watu wa rangi tofauti, na bweni ambalo tukio hilo la kuwadhalilisha wafanyakazi hao weusi, lipo karibu na hapo.

'Bweni hilo ni kama kumbukumbu kwa taasisi yetu kuhusu changamoto tunayokabiliana nayo na kuna kazi nyingi ya kufanya' alisema John Samuel mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Miezi michache iliyopita wanafunzi walioweka video hiyo kwenye intaneti, walitozwa faini na mahakama kuu walipokutwa na hatia ya kufanya tabia ya kihalfu.

Image caption Ubaguzi ulizusha ghasia Afrika Kusini

Sasa, chuo hicho kinatumia tukio hilo kama msukumo wa kuleta mabadiliko ukiongozwa na makamu mkuu wa chuo hicho.

Hapo awali, kulikuwa na tatizo la watu weusi na watu weupe lakini sasa matazamo wa wengi umeanza kubadilika; sio kwamba hakuna mambo mabaya ambayo yanatendeka lakini mambo mazuri pia yanaendelea.

Wamechanganyika

Miaka miwili iliyopita ubaguzi wa rangi ulikuwa katika hali ya juu kiasi kwamba hata mabweni ya wanafunzi weusi yalikuwa tofauti na wanafunzi wazungu.

Sasa katika mabweni hayo 23, wanafunzi wote wanaishi pamoja wakiwa wamechanganyika.

Profesa Jonathan Jansen wa chuo hicho alisema 'sijaamnini kuwa mabadilkio haya yamekuja haraka hivi.'

Image caption Jimbo la Free State

Uchunguzi uliofanywa miaka miwili iliyopoita ulibaini kwamba asilimia 42 ya wanafuzi wazungu walipinga pendekezo la kuishi pamoja na wanafuzi weusi; na sasa baada ya kuanzisha mpango wa kujumuisha wanafunzi wote katika mabweni, baadhi yao wamehamia mjini kupinga mswada huo, lakini ni wachache.

Chuo hicho kimepiga hatua kubwa sana katika mfumo huo wa kuwaleta pamoja watu wa rangi tofauti lakini katika uwanja wa michezo, imekuwa vigumu sana kuwachagiza wanafunzi kukubali hatua hii.

Image caption Mmoja wa wafanyakazi wa chuo kikuu waliodhalilishwa

Mwanafunzi mmoja kutoka jamii ya Afrikaans, Franco Van De Merwe, alisema 'Watu hawana budi kukubali kwamba zama za ubaguzi zimeisha na ikiwa wanataka heshima, inabidi waende na wakati. Ni jambo la uvumilivu.'

'Ninatambua kwamba kuna baadhi ya wanafuzi waliohamia mjini kwa sababu hawafurahii kuwa pamoja na watu weusi. Hili ni tatizo lililoanzishwa na vizazi vya kale na Kwa bahati mbaya, fikra hizo zimekumba kizazi kipya. Tatizo hili halitawahi kutokomezwa.'