Jeshi lafuta bunge Misri

Utawala mpya wa kijeshi nchini Misri umesema unalifunga bunge la kuisimamisha katika ya nchi kwa muda.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji mjini Cairo

Katika taarifa kupitia televsheni ya taifa, baraza la juu la kijeshi limesema litakaa madarakani kwa miezi sita, au mpaka wakati utakapofanyika uchaguzi.

Bunge la sasa la Misri, limetawaliwa na wafuasi wa Rais Hosni Mubarak, ambaye aliondoka madarakani siku ya Ijumaa, kufuatia siku 18 za maandamano.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji katika eneo la wazi la Tahrir

Mapema kulikuwa na mzozano katika eneo la wazi la Tahrir, baada ya waandamanaji kugomea hatua za jeshi za kuwaondoa katika eneo hilo.

Polisi wa kijeshi wametaka mahema kuondolewa katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha maandamano yaliyosababisha kuondoka kwa Bw Mubarak.

Mwandishi wa BBC Wyre Davis aliyeko mjini Cairo anasema hali katika eneo hilo la wazi imekuwa kama mvutano wa kirafiki, lakini wandamanaji wamesema wataendelea kusalia hapo hapo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wa kijeshi wakiwa na waandamanaji

Taarifa ya jeshi ilioyosomwa kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumapili imesema itasitisha katiba iliyopo na kuunda kamati itakayoandika muswada mpya wa katiba, kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Katiba ya sasa inazuia vyama ving vya kisiasa na makundi kushiriki katika uchaguzi, na hivyo kufanya bunge la nchi hiyo kujaa wafuasi wa chama cha National Democratic, ambacho kinamtii Bw Mubarak.

Mwandishi wetu anasema, tangazo hili jipya linamaanisha uchaguziutafanyika mwezi Julai au Agosti, badala ya Septemba kama ilivyokuwa imepangwa.