Benki zafungwa tena Misri

Haki miliki ya picha Other
Image caption Uwanja wa Tahrir mjini Cairo

Benki nchini Misri zimelazimika kufungwa kwa mara nyingine tena kutokana na maandamano ya kupinga ufisadi

yaliyofanywa na wafanyikazi katika taasisi za serikali.

Haya yanajiri wakati viongozi wa kijeshi wakijaribu kuwashawishi wananchi wa Misti kurejea kazini baada ya maandamano yaliyomngoa madarakani rais hosni Mubarak.

Siku ya jumapili,Baraza kuu la utawala wa kijeshi lilivunjilia mbali bunge na kuahirisha utawala wa katiba ambayo ilivinyima vyama vya kisiasa kushiriki katika uchaguzi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi wa Misri

Jeshi pia limesema litashikilia madaraka kwa kipindi cha miezi sita na kisha kuandaa uchaguzi mkuu.

Huku hayo yakiarifiwa wengi wa waandamanaji wameondoka katika uwanja wa tahrir katikati mwa jiji la Cairo.

Hata hivyo kundi dogo la waandamanaji wenye msimamo mkali bado linaendelea kupiga kambi katika eneo hilo.