Wahamiaji 50 wafa maji Msumbiji

Wahamiaji haramu
Image caption Wahamiaji haramu

Wahamiaji haramu 50 raia wa Somalia wanahofiwa kufa maji, baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Msumbiji hivi karibuni.

Msemaji wa polisi nchini Msumbiji, amethibitisha nahodha wa meli hiyo ya Tanzania ni miongoni mwa waliozama katika kisiwa cha Suhavo Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wahamiaji wengine 80 kutoka Somalia na Ethiopia walionusirika ajali hiyo wamepelekwa katika kambi moja ya wakimbizi mkoa wa Nampula nchini Msumbiji.

Waandishi wa habari wanasema Msumbiji imekuwa njia muhimu kwa wahamiaji haramu wanaotoka Somalia, India na China kuelekea nchini Afrika Kusini.