Polisi wakabiliana na waandamanaji Bahhrain

Waandamanaji nchini Bahrain Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji nchini Bahrain

Maafisa wa usalama katika Himaya ya Bahrain wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga Serikali ambao wamepiga kambi katika bustani kati kati mwa mji mkuu wa Manama.

Walioshuhudia maandamano hayo wanasema polisi waliwasili wakati waandamanaji walikuwa wakijiandaa kulala.

Makundi ya upinzani yanasema kuwa watu wawili walifariki na wengine wengi kujeruhiwa.

Wanasema polisi waliwasili mahala hapo na kuanza kuwarushia mabomu ya kutoa machozi na wakati huo huo kufyatua risasi za mipira; jambo lililowafanya watu kukimbilia mitaa iliyo karibu.

Jana maelfu ya waandamanaji walishiriki kwenye maandamano ya kupinga serikali kwa siku ya tatu mfululizo katika mji mkuu wa Manama.