United yapenya Kombe la FA

Manchester United imepenya kuingia robo fainali ya kombe la FA baada ya kuifunga timu ya daraja la chini, Crawley Town kwa goli 1-0.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Crawley Town FC

Goli hilo pekee la United limefungwa na Wes Brown katika dakika ya 28.

Crawley waliipa United wakati mgumu, na hata kufikia kugonga nguzo ya juu katika dakika za majeruhi kupitia mchezaji Richard Brodie.

Image caption Nahodha Wes Brown alifunga bao pekee na la ushindi

Manchester walionekana kupwaya katika safu ya ushambuliaji iliyokuwa na Bebe na Gabriel Obertan na Xavier Hernandez.

Kipindi cha pili licha ya United kumchezesha Wayne Rooney, Crawley Town ilitawala mchezo, lakini haikuweza kufanikiwa kupata goli.

Katika michezo mingine Birmingham City imeinyuka Sheffield Wednesday mabao 3-0, na Stoke City kuichapa Brighton 3-0.