Maandamano kuipinga serikali ya Bahrain

Maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Bahrain wamerejea katika uwanja wa "Lulu" (Pearl Square,) ambako ndio kitovu cha maandamano katika mji mkuu Manama.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji nchini Bahrain

Waandamanji waliojawa na furaha walirejea katika eneo hilo baada ya polisi wa kutuliza fujo kufyatua gesi ya kutoa machozi na risasi hewani kabla ya kuondoka.

Taarifa zaeleza takriban watu 60 huenda wamejeruhiwa.

Jeshi ambalo lilikua likiulinza uwanja huo baada ya kutumia nguvu kuwatimua waandamanaji siku ya Alhamisi, liliarishwa liondoke.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Bahrain likishika doria

Mrithi wa kifalme wa Bahrain ameanza kuzungumza na vyama vya upinzani, mkiwemo vyama vikuu vya upinzani vinavyoungwa mkono na wafuasi wa madhehebu ya Shia katika dola hiyo ya ghuba inayotawaliwa na ukoo wa kifalme wa madhehebu ya Sunni.

Kwa mujibu wa mwaandishi wa BBC Caroline Hawley aliyoko huko mjini Manama.

Ripoti za hapo awali zilieleza kwamba kundi kuu la upinzani la wafuasi wa Kishia , Wefaq, lilikataa pendekezo la mfalme la kufanya mazungumzo ya kujaribu kukomesha machafuko hyaliyoendelea kwa muda wa siku nane.

Kilidai kuondolewa kwa wanajeshi kutoka mitaani kabla ya kuanza mazungumzo yoyote.