Amri ya kutotoka nje yatolewa na Gbagbo

Hapo jana Bwana Gbagbo aliweka amri ya kutotoka nje kwa siku tatu baada ya wafuasi wa Bwana Ouattara kutoa wito kufanywa mapinduzi kama yale ya Misri.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waandamanaji nchini Ivory Coast

Tangazo hilo limejiri baada ya wafuasi wa Alassane Ouattara, mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani katika uchaguzi wa mwaka uliopita, kuitisha mapinduzi ya kiraia kama yaliyotokea nchini Misri.

Mamia ya watu walikusanyika mjini Abidjan kutaka rais wa sasa, Laurent Gbagbo akabidhi madaraka kwa Bwana Ouattara.

Habari zaidi zinansema kuwa askari wa usalama wa Ivory Coast wametumia mabomu ya kutoza machozi dhidi ya wafuasi wa Alassane Ouattara ambaye anatambuliwa kuwa mshindi wa uchaguzi rais wa mwaka jana.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bw Ouattara

Bwana Ouattara anatambuliwa na jamii ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais lakini rais wa sasa, Laurent Gbagbo, amekataa kuondoka madarakani.

Benki za mataifa ya kigeni zimearisha shughuli zake nchini Ivory Coast lakini bwana Gbagbo ametishia kuzitaifisha.

Mauzo katika mataifa ya ng'ambo ya zao la coacoa ambalo hukuzwa nchini humo kwa wingi yamepigwa marufuku na Ivory Coast inakabiliwa na tishio la kutumbukia katika mgogoro wa kiuchumi kama ule ulioshuhudiwa nchini Zimbabwe.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wafanyikazi wakikagua cacao