Luteni Kanali Kibibi afikishwa mahakamani

Waathiriwa wa ubakaji nchini Congo Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waathiriwa wa ubakaji nchini Congo

Mwendesha mashtaka mmoja nchini Congo, ametoa wito mahakama nchini humo kutoa adhabu ya kifo kwa wanajeshi watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na visa vya ubakaji na uhalifu dhidi ya binadam.

Wanajeshi wengine watano huenda wakahumukiwa kifungo cha hadi miaka 20 gerezani.

Afisa huyo mwandamizi anayekabiliwa na mashtaka ni Luteni Kanali Daniel Kibibi, ambaye anatuhumiwa kuidhinisha wanajeshi wake kuwadhulumu kina mama na watoto mjini Fizi, Mashariki mwa Congo mwezi uliopita, kulipisa kisasi kuauwa kwa mmoja wao.

Kibibi amekanusha mashtaka hayo na kusema wao walikuwa wakijaribu kuthibiti machafuko yaliyokuwa yamedumu kwa zaidi ya saa 9 mjini Fizi.

Waendesha mashtaka wanasema karibu wanajeshi wote 150 waliokuwa chini ya Luteni Kanali Kibibi, walitekeleza uhalifu huo.