Rais Yoweri Museveni ashinda uchaguzi wa urais

Tangazo rasmi limetolewa kuthibitisha kuwa Rais Museveni ndiye mshindi katika uchaguzi uliofanywa Ijumaa.

Image caption Rais Yoweri Museveni

Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Yoweri Museveni alishinda kwa asilimia 68, katika uchaguzi huo uliofanyika Ijumaa, naye mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alipata kura asilimia 26.

Bw Besigye amekataa kukubali matokeo hayo na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika shughuli ya uchaguzi.

Chama kilicho madarakani kimetuhumiwa kwa kutumia rasilmali ya serikali kuwahonga wapigaji kura.

Uchaguzi huo uliendelea kwa utulivu ingawaje kuna ripoti za vurugu kadhaa baina ya wafuasi wa chama kinachotawala na chama cha upinzani.