'Utulivu' Libya

Barabara za mji mkuu wa Libya Tripoli, zimeripotiwa kuwa kimya baada ya ghasia usiku wa makabiliano kati ya wapinzani wa serikali na wafuasi wa rais Muamar Gaddafi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji leo wametulia nchini Libya

Hata hivyo milio ya risasi bado ilikuwa inasikika hadi kufikia saa za asubuhi leo.

Mwanawe rais Gaddafi alithibitisha kupitia runinga ya taifa kuwa miji mwiili mashariki mwa Libya Benghazi na Bayda imetawaliwa na upinzani.

Alionya dhidi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe akisema kuwa wafuasi wa babake watampigania katika hali yoyote.

Hata hivyo upinzani nao umeahidi kuhakikisha kuwa rais Muamar Gadaffi anaondoka mamlakani.

Mjumbe wa Libya katika Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Abdel Moneim al-Honi, ametangaza kwamba anajiunga na mageuzi hayo, na balozi wa Libya nchini India, Ali al-Essawi amesema anajiuzulu kutokana na serikali yake kutumia nguvu katika kupambana na waandamanaji.

Mohamed Bayou, na ambaye ni mwezi mmoja tu umepita tangu kuacha kuwa msemaji wa serikali ya Libya, amesema uongozi wa nchi hiyo umekosea katika kuwatisha waandamanaji kwa kutumia nguvu.