Angola yatinga fainali CHAN

Angola imeingia fainali ya michuano ya CHAN baada ya kuichapa wenyeji Sudan kwa mikwaju ya penati.

Angola walipata penati 4, huku Sudan wakipata 2, baada ya dakika 90, na muda wa ziada kumalizika timu hizo zikiwa nguvu sawa ya 1-1.

Mchezo huo ulizongwa na mizengwe kutoka kwa mashabiki wa Sudan, ambao walitupa chupa uwanjani kufuatia matokeo hayo.

Saifeldin Ali Idris wa Sudan aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, lakini dakika 20 kabla ya kumalizika kwa mchezo Arsenio Cabungula alisawazisha bao hilo.

Angola walitakiwa kupatiwa penati kabla ya mchezo kumalizika, baad ya kipa wa Sudan kupewa kadi nyekudu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Angola, lakini mwamuzi hakuchukua hatua zaidi ya kutoa kadi.

Kwa ushindi huo, Angola itacheza fainali na Tunisia Februari 25.