Wanajeshi wa Gbagbo wauwawa Ivory Coast

Haki miliki ya picha afp
Image caption Wanajeshi wa Ivory Coast

Wanajeshi wasiopungua 10 watiifu kwa kingozi aliyekatalia madarakani nchini Ivory Coast, Laurent Gbagbo, wanaripotiwa kuuwawa katika vurungu katika mji mkuu wa nchi hiyo Abidjan.

Ripoti kutoka nchini humo zinasema, wanajeshi wa Bw Laurent Gbagbo walishambulia eneo linalo muunga mkono kiongozi anayetambulika na jamii ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa mwaka uliopita, Alassane Ouattara.

Walioshuhudia wanasema wanajeshi watiifu kwa rais Gbagbo waliwapiga risasi wafuasi wa Bw Ouattara, na kuwauwa watu sita.

Vifo hivyo vinatokea huku jaribio la hivi karibuni la viongozi wanne wa Afrika likiendelea kujaribu kutafuta suluhu la mzozo nchini Ivory Coast.