Liverpool yasonga mbele Ulaya

Goli la kichwa katika dakika za lala salama limeipeleka Liverpool katika ngazi ya timu 16 katika michuano ya Kombe la Europa dhidi ya Sparta Prague.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Ushindi wa kwanza Ulaya kwa Daglish

Bao hilo limefungwa na Dirk Kuyt katika dakika ya 86, kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Raul Meireles.

Katika mchezo wa mwanzo timu hizo mbili zilitoka sare.

Rangers nayo ya Scotland ilisonga mbele kwa goli la ugenini baada ya kutoka sare ya 3-3 na Sporting.

Katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Rangers.