Huwezi kusikiliza tena

Mjadala wa mabomu Tanzania

Je ni salama kwa wananchi kuishi karibu na kambi za jeshi??

Nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam, kwa mara nyingine kulitokea milipuko ya mabomu katika ghala la kuhifadhi silaha la jeshi la Wananchi wa Tanzania, iliyopo Gongo la Mboto ambapo watu 20 kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jemedari Abdulrahaman Shimbo, walifariki dunia na wengine zaidi ya 100 walijeruhiwa.

Ni tukio la pili kama hilo baada ya miaka miwili katika kambi ya wanajeshi wa Tanzania iliyopo Mbagala nako kulirindima mabomu yaliyokuwa yakiruka hadi katika makazi ya raia. Katika mjadala tutajadili je ni salama kwa watu kuishi karibu na kambi za jeshi?