Huwezi kusikiliza tena

Mmiliki wa Dowans

WAKATI Mjadala wa kampuni yenye vinu vya kufua umeme, Dowans ukibaki kwenye swali la nani mmiliki wake nchini Tanzania, raia wa Oman, amejitokeza na kukiri kuimiliki kampuni hiyo inayoidai serikali ya Tanzania mabilioni ya fedha. Mtu huyo alikutana na wahariri wa vyombo vya habari vya Tanzania alivyochagua.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Charles Hilary alizungumza na mwandishi wa habari ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Citizen Bakari Machumu aliyekuwepo katika mkutano huo na waandishi wa habari, kufahamu zaidi juu ya mmiliki huyo wa kampuni ya Dowans.