Assange kufikishwa Sweden

Jaji katika mahakama moja kusini mwa mji wa London, Uingereza, ameamua kwamba mwanzilishi wa tovuti ya WikiLeaks, inafaa afikishwa nchini Sweden, kwa mashtaka dhidi ya ubakaji.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Assange anasema utaratibu unaotumia kuwasafirisha watuhumiwa Ulaya haufai

Hata hivyo Julian Assange anakanusha mashtaka hayo.

Wakili wake amesema watakata rufaa kuhusu uamuzi uliopitishwa Alhamisi.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Bw Assange amesema utaratibu wa kuwahamisha washtakiwa barani Ulaya kutoka nchi moja hadi nyingine unafaa kuchunguzwa upya.