Tunisia yashinda CHAN

Tunisia wameshinda kombe la CHAN, baada ya kuwafunga Angola kwa mabao 3-0.

Image caption Timu ya Angola

Tunishia wameshinda michuano hiyo ya wachezaji wasiocheza nje ya bara la Afrika katika fainali iliyochezwa nchini Sudan siku ya Ijumaa.

Baada ya nusu ya kwanza iliyodorora, Tunisia walizinduka na kupachika mabao hayo matatu katika kipindi cha pili.

Wanakuwa mabingwa wa pili wa michuano hiyo, baada ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuwa ya kwanza kunyakua ubingwa huo miaka miwili iliyopita.

Image caption DR Congo, washindi wa CHAN 2009

Medji Traoui alipata bao la kwanza dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili.

Licha ya Angola kuwa na sifa ya kuweza kudhibiti vyema katika safu ya ulinzi walishindwa kuzuia bao la pili lilifungwa na Zouhaier Dhaouiadi, dakika 15 kabla ya kumalizika kwa mchezo.

Dakika tano baadaye, mchezaji wa akiba aliyeingia Ousama Darragi alipachika bao la tatu.

Mchezo huo uliochezwa Omdurman, ulichezwa mbele ya uwanja ambao haukuwa umejaa, na kufuatiwa na sherehe maridadi za kufunga michuano hiyo.