Arsenal kumkosa Van Persie kwa wiki tatu

Mshambiliaji hatari wa Arsenal, Robin van Persie, atakosa mchezo wa marudio dhidi ya Barcelona kuwania Ubingwa wa soka kwa vilabu vya Ulaya, tarehe 8 mwezi huu wa Machi, baada ya kuumia goti.

Image caption Robin van Persie akitibiwa uwanjani

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu ya Arsenal iliyotolewa kupitia mtandao wao, van Persie hatacheza soka kwa muda wa wiki tatu.

Van Persie uliumia goti siku ya Jumapili wakati wa fainali ya Kombe la Carling, ambapo Arsenal ilifungwa 2-1 na Birmingham.

Hayo yakiwa yanatokea, mshambuliaji mwengine wa pembeni wa timu hiyo, Theo Walcott naye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.

Kuwakosa washambuliaji hao wawili, kutaathiri nafasi ya Arsenal kutetea ushindi wake wa mabao 2-1 iliyoupata katika mechozo wa awali.

Lakini taarifa hiyo ya Arsenal imesema, kuna "uwezekano" wa nahodha wake Cesc Fabregas anayesumbuliwa na maumivu ya msuli wa paja, akacheza katika mechi hiyo dhidi ya Barcelona.