Bomu lajeruhi 10 Rwanda

Kagame
Image caption Rais Kagame wa Rwanda

Watu 10 wanejeruhiwa nchini Rwanda baada ya bomu kulipuka katika kituo cha basi mjini Kigali. Polisi wamesema hawajakamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hilo.

Mlipuko huo umetokea katika kituo cha basi kilichopo kwenye makutano ya barabara za Kimisagara na Nyakabanda.

Mlipuko huo ulilenga abiria waliokuwa wakiingia ndani ya basi la abiria.

Upelelezi bado unaendelea, wamesema polisi.

Mwandishi wa BBC mjini KIgali, Yves Bucyana anasema hata hivyo polisi wamekamata watu watano kuhusiana na matukio mengine ya milipuko ya mabomu nchini humo.

Polisi walisema mshukiwa mmoja alikamatwa akiwa na mabomu mawili, kati ya 15 anayodai alipewa nchini Burundi, katika mtandao wa walipuaji mabomu mjini Kigali.

Watuhumiwa hao sasa wanaongeza idadi ya watuhumiwa wa walipuaji mabomu. Tayari watu 29 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Wengi wamekiri kuhusika na vitendo hivyo wakidai kuwa waliatumwa na kundi la FDLR.