Umeme na Maji zakatwa Ivory Coast

Ramani ya Ivory Coast

Afisa wa Umoja wa mataifa nchini Ivory Coast amethibitisha kuwa huduma za maji na umeme zimekatwa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Eneo hio linampinga Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kuachia madaraka licha ya jamii ya kimataifa kukubaliana kuwa alishindwa katika uchaguzi wa Novemba mwaka uliopita.

Afisa huyo wa umoja wa mataifa , Ndolamb Ngokwey, amesema kampuni ya umeme ya Ivory Coast imemuarifu kuwa huduma hizo zimekatwa kwa misingi ya kisaisa na hakukua na matatizo ya kimitambo.

Umeme ni muhimu katika eneo hilo la mashambani na hutumika kusambaza maji kutoka kwa mabwawa.