Toure anatumia "dawa"

Beki wa Manchester Kolo Toure amesitishwa kucheza soka baada ya kupimwa na kugundua alitumia dawa inayotambuliwa, specified substance.

Image caption Kolo Toure

Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 29, aliarifiwa na chama cha soka cha England, FA, kwamba iligunduliwa alitumia dawa hiyo mwezi uliopita, wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Manchester United, na yeye akiwa ni mchezaji wa zamu, licha ya kutopewa nafasi kucheza katika mechi hiyo.

Shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku World Anti-Doping Agency, WADA,' lilisema dawa hiyo ni mojawapo ya dawa zinazoweza kutumiwa kama dawa ya kawaida tu na basi sio mojawapo ya zile zilizopigwa marufuku.

Adhabu inayoweza kutolewa na shirika la kimataifa la kuzuia utumizi wa madawa ya kuongezea nguvu michezoni, WADA, haijulikani.

Huenda likatoa onyo, ama kumuadhibu kwa kumpiga marufuku asicheze kwa kipindi cha hata miaka miwili.

Image caption Kolo Toure upande wa kulia

Shirika hilo limeelezea kwamba limemsimamisha asicheze baada ya kugundua alitumia specified substance, likimaanisha kwamba licha ya ushahidi kupatikana kwamba alitumia dawa hiyo, huenda ikawa sio kupitia njia ya moja kwa moja ya kuitumia kama dawa ya kuongezea nguvu michezoni, lakini huenda ikawa mwilini kupitia njia nyinginezo.

Klabu ya Manchester City imethibitisha kwmaba Toure amesitishwa kucheza soka, huku wakisubiri utaratibu wa kisheria utakwenda vipi.

Toure ana hadi tarehe 9 Machi kuamua iwapo anataka sampuli ya pili ipimwe.

Lakini, iwapo hatapimwa tena basi itabidi akabidhi maelezo na atakabiliwa na taratibu ya adhabu itakayochukua muda mrefu.