Watu watatu wauawa mlipuko Nigeria

Mlipuko wa bomu umetokea katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na watu wasiopungua watatu waliuwawa kwa mujibu wa polisi wa nchi hiyo.

Image caption Ramani ya Nigeria

Maafisa walisema mlipuko huo ulitokea katika mhadhara wa chama cha Peoples Democratic Party huko Suleja, kilomita 40 kutoka Abuja.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Katikati mwa nchi hiyo kumeibuka vurugu kati ya makundi ya kikabila, kidini na ya kisiasa.

Msemaji wa polisi Olisola Amore alisema bomu hilo lilirushwa kutoka kwenye gari moja lakini haikufikia katikati mwa maandamano hayo na kuanguka karibu na soko iliyokuwa karibu.

Watu watatu waliuawa papo hapo na wengine 21 walijeruhiwa.

Alisema kuwa hakuna kundi lolote ambalo limejihusisha na shambulio hilo na hakuna aliyekamatwa..

Bw Amore alisema mgombea wa urais wa chama hicho cha PDP, Babangida Aliyi, hakujeruhiwa.

Yushua Shuaib msemaji wa shirika la taifa la utawala wa dharura, NEMA, alisema kuwa shambulio hilo lilitokea baada ya maandamno hayo kumalizika.