Mashindano ya Euro 2012 wamuzi watano

Watunga sheria za soka, wameamua kutumia waamuzi watano wakati wa fainali za mashindano ya Euro 2012, na wataendelea na majaribio ya kutumia teknolojia langoni kuamua mpira umeingia au la.

Image caption Fainali za Euro 2012

Bodi ya Kimataifa ya Soka, imetoa uamuzi huo baada ya kikao chao cha mwaka kilichofanyika Newport, Wales siku ya Jumamosi.

Matumizi ya waamuzi wawili wa ziada, umefuatia majaribio yaliyofanyika katika Kombe la Europa, wakati teknolojia ya langoni ilishindwa katika majaribio ya hivi karibuni na majaribio mengine yataendelea baadae mwaka huu.

Katika uamuzi mwengine wachezaji watafungiwa pia imeamuliwa watafungiwa kucheza soka iwapo wataendelea kuvaa skafu nzito ya kuzuia baridi inayovaliwa shingoni ama kuanzia mwezi wa Julai wakiwa uwanjani.