United yaangukia pua, tena

Liverpool imeichapa Manchester United kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Anfiled.

Dirk Kuyt alifunga mabao yote hayo matatu katika mchezo uliotwaliwa zaidi na Liverpool.

Mabao hayo yalifungwa katika dakika za 34, 39, na 65.

Bao pekee na la kufutia machozi lilifungwa na Havier Hernandez katika dakika ya 90.

United wanasalia kileleni wakiwa na pointi 60, huku Liverpool wakiisogelea Tottenham kwa kufikisha pointi 42, huku Spurs wakiwa na 47.