United yain'goa Arsenal FA

Manchester United imeichapa Arsenal 2-0 na kutinga katika nusu fainali ya michuano ya kombe la FA.

Magoli ya Fabio Da Silva na Wayne Rooney yalitosha kuiondoa Arsenal katika michuano hiyo.

Fabio aliandika bao la kwanza katika dakika ya 28, huku Wayne Rooney akifunga bao la pili katika dakika ya 49.

Katika mchezo wa awali Bolton iliichapa Birmingham City kwa mabao 3-2.