Sudan Kusini yashuku njama

Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa inasimamisha mazungumzo na Sudan Kaskazini na imemshutumu Rais Bashir kuwa anapanga njama ya kuipindua serikali ya kusini kabla ya uhuru, mwezi Julai.

Image caption Pagan Amun, kulia

Afisa mwandamizi, Pagan Amun, alisema Rais Bashir anasimamia njama inayotekelezwa na idara ya ujasusi ya jeshi.

Pia alisema serikali ya Sudan Kusini, inachunguza njia nyingine ya kusafirisha mafuta, badala ya kupitia Sudan Kaskazini kama ilivyo hivi sasa.

Tamko hilo lilitolewa baada ya ripoti za shambulio, lilofanywa alfajiri dhidi ya mji wa Malakal, linalofikiriwa kufanywa na wafuasi wa afisa aliyeasi wa Sudan Kusini, George Athor.