Mji wa Abidjan ni shuwari

Utulivu umerejea Abidjan siku moja baada ya mapigano makali katika kitongoji cha Abobo.

Image caption Ramani ya Ivory Coast

Taarifa kutoka Ivory Coast zinaeleza kuwa mji wa Abidjan ni shuwari, siku moja baada ya mapigano makali, katika kitongoji cha Abobo, kinachodhibitiwa na wafuasi wa Alassane Ouattara anayetambuliwa kimataifa kuwa rais.

Taarifa hizo zinasema kuwa watu kadha waliuwawa wakati eneo hilo liliposhambuliwa na askari wa mpinzani wa Bwana Ouattara, Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kuacha madaraka ingawa alishindwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka jana.

Umoja wa Mataifa ulisema, afisa wake mmoja kutoka Ghana alijeruhiwa wakati gari lake liliposhambuliwa na vijana mjini Abidjan.