10,000 wahofiwa kufariki dunia Japan

Juhudi za ukombozi zinaendelea Japan na katika eneo moja lilopigwa na tsunami, inahofiwa watu kama elfu kumi wamekufa.

Haki miliki ya picha Reuters (audio)
Image caption Juhudi za ukombozi Japan

Wakuu wa Japani wameonya kwamba kunaweza kutokea mripuko mwingine kwenye kinu cha nishati cha nyuklia kaskazini mwa mji wa Tokyo wakijaribu kuzuwia tanuri ndani ya kinu kuripuka.

Wamekiri kuwa miyale ya nyuklia karibu na kinu hicho kilioko Fukushima wakati mmoja ilizidi kiwango kinachofikiriwa kuwa salama baada ya kinu hicho kuharibika katika tetemeko kubwa lilotokea Ijumaa.

Wahandisi wamejaribu na kushindwa kupooza tanuri katika kinu kimoja kwa kutumia maji ya chumvi.

Lakini wanafikiri pipa linalofunika tanuri ni imara na litahimili mripuko kwa hivyo miyale haitovuja.

Jana kulitokea mripuko mkubwa kwenye kinu kimoja cha Fukushima.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jeshi likitoa msaada wa dharura kwa raia wa Japan