Jeshi limeukomboa mji wa Brega, Libya

Televisheni ya Libya inasema kuwa jeshi limeukomboa mji wa Brega ulioko mashariki kutoka wale walioelezewa kuwa magenge yenye silaha.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Hali nchini Libya

Taarifa hizo hazijaweza kuthibitishwa.

Majeshi ya Gaddafi yamekuwa yakisonga mbele kwa kasi dhidi ya wapiganaji wasiokuwa na silaha wala uongozi mmoj, katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa nchi.

Kukombolewa kwa mji mdogo wa Brega, kama ni kweli, kutathibitisha mkondo ambao umejitokeza katika siku chache zilizopita.

Jeshi la Gaddafi limeweza kugeuza mafanikio ya wapiganaji waliyoyapata wakati upinzani ulipoanza.

Wapiganaji wanasema wanarejeshwa nyuma kwa sababu nguvu zao na zile za upande wa Gaddafi hazilingani.

Wanasema wanashambuliwa na ndege na manuwari na wanataka jumuiya ya kimataifa kufanya haraka kuweka amri ya kuzuwia ndege kuruka katika anga ya Libya ili kupunguza uwezo wa serikali.

Lakini Kanali Gaddafi amelitoa maanani tishio la kuingiliwa kati.

Inavoelekea yeye na wapinzani wake wako tayari kupigana hadi mwisho.