Ferguson ahukumiwa na FA

Chama cha soka cha England, kimemfungia Sir Alex Ferguson mechi tano kocha kwa kauli alizotoa kuhusu mwamuzi Martin Atkinson.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Martin Atkinson

Kocha huyo wa Manchester United amepatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kwa kukosoa ufanisi wake alipochezesha mechi kati ya Chelsea na Man U mapema mwezi huu, mechi ambayo United waliambulia kipigo.

Adhabu hiyo inaanza tarehe 22 mwezi huu na itahusisha mechi ya kombe la FA dhidi ya mahasimu wao Manchester City. Sababu za uamuzi huo zitatumwa kwa Ferguson katika muda wa saa 24 zijazo kisha atakuwa na saa nyingine 48 kuamua endapo anataka kukata rufaa.