Tahadhari kwenye mtambo wa nyuklia Japan

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Tsunami, Japan

Fundi mitambo wanahangaika kudhibiti kinu cha tatu cha kinyuklia katika mtambo wa nyuklia kilichokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi, ambalo limetikiswa na mlipuko wa pili katika kipindi cha siku tatu.

Vyuma vya mafuta vilivyopo ndani ya kinu hicho kwenye mtambo wa Fukushima Daiichi vimefunuliwa katika nyakati mbili tofauti, na kuzua wasiwasi wa kuyeyuka.

Maji ya baharini yamekuwa yakitiwa kwenye kinu hicho ili kuzuia kupashika joto kupita kiasi.

Kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa kupunguza joto kulianza kabla ya milipuko kutokea kwenye mtambo namba 3 na mtambo namba 1 siku ya Jumamosi

Mlipuko uliotokea hivi karibuni ulijeruhi watu 11, na mmoja ameumia sana.

Mlipuko huo ulitikisa umbali wa kilomita 40 kutoka ulipotokea na kusababisha moshi mkubwa hewani.

Jengo lililokuwa nje ya mtambo huo uliharibika sana.