Mtambo wa Nyuklia walipuka Japan

Mtambo wa Nyukilia japan walipuka Haki miliki ya picha BBC World Service

Kumetokea mlipuko mwingine katika kinu cha kinukilia kilichoharibiwa na tetemeko la ardhi cha mji wa Fukushima. Mlipuko huo ulitifua moshi mkubwa katika eneo hilo.

Mlipuko huo wa hewa ya Hydrogen ulitokea katika mtambo wa tatu, lakini katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan amesema kuwa hakuna hatari ya kusababisha kuvuja kwa sumu ya kinukilia kutokana na mlipuko huo ni ndogo sana.

Msimamizi wa kiwanda hicho amesema kuwa mlipuko huo haujaharibu kifaa kinacho hifadhi mtambo huo wa kinukilia. Kiwanda hicho kinasema watu sita walijaruhiwa.

Hadi kufikia sasa watu 22 wametibiwa kutokana na madhara ya kuharibika kwa kinu hicho cha kinukilia. Awali Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan, alisema kuwa kinu hicho kilichoharibiwa kutokana na uharibifu wa Ijumaa kilikuwa katika hali ya hatari. Mlipuko wa hewa ya hydrogen ulirusha hewani paa la sehemu moja ya kiwanda mnamo Jumamosi. Mitetemeko midogomidogo imeendelea kutokea maeneo kadhaa nchini humo.