Majeshi ya Gaddafi yawashambulia waasi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waasi wakiwa mjini Ajdabiya

Majeshi ya Kanali Muammar Gaddafi's yanasogea taratibu kwenye miji inayoshikiliwa na waasi nchini Libya.

Ajdabiya, mji mkuu wa mwisho kabla ya kufika eneo linalokhodhiwa na waasi la Benghazi, mashariki mwa Libya, limejikuta likishambuliwa kupitia angani.

Na huko magharibi, majeshi ya ardhini na vifaru vimekuwa vikiushambulia mji wa Zuwara.

Awali, majeshi ya waasi yalisema yaliudhibiti tena mji wa Brega, lakini serikali imepuuzilia mbali madai hayo.

Wakati huo huo, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linafikiria kutoa amri ya kupiga marufuku upitaji wa ndege kwenye anga ya Libya.

Jumuiya ya kiarabu iliunga mkono hatua hiyo siku ya Jumamosi, lakini majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato na Marekani mpaka sasa imeonyesha wasiwasi wa kuhusisha jeshi moja kwa moja katika mgogoro huo.