Issoufou ashinda uchaguzi wa urais Niger

Tume ya uchaguzi nchini Niger imetangaza kuwa kiongozi wa upinzani nchini Niger Mahamadou Issoufou ameshinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 58 ya kura.

Image caption Mahamadou Issoufou

Bw Issoufou aliwahi kushindwa na aliyekuwa rais, Mamadou Tandja, mara mbili katika uchaguzi za hapo awali.

Seini Oumarou mgombea wa kiti cha urais kutoka chama cha MNSD ambacho ni chama cha Bw Tandja, alipata kura aslimia 42.

Uchaguzi huo inatazamiwa kurudisha hali ya utawala wa raia katika nchi hiyo.