Waziri ajiuzulu nchini Uganda

Wafuasi wa NRM Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri Buturo alihama chama twala NRM baada kushindwa kwenye kura za mchujo

Aliyekuwa waziri wa maadili nchini Uganda, Dr Nsaba Buturo amejiuzulu wadhfa wake kufuatia uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini humo.

Mahakama hiyo imeamuru kuwa wanasiasa wanaohama vyama vyao vya kisiasa na kujiunga na vingine wakiwa bado wanahudumu kama wabunge wafutwe kazi.

Katiba ya sasa nchini Uganda inasema kuwa mbunge yeyote akitaka kuhama chake na kujiunga na kingine ni sharti ajiuzulu kwanza wadhfa wake na uchaguzi mdogo kuandaliwa.

Dr Buturo alisema, "kilichobakia kwangu kilikuwa kuondoka afisini na heshima yangu yote."

Chini ya sheria mpya, ambayo ingawa ipo-haijatekelezwa, zaidi ya Wabunge 70, kukiwemo Mawaziri tisa wanapaswa kujiuzulu, sio tu Uwaziri lakini pia viti vyao vya Bunge.

Wanasiasa hao wakitaka kurejea tena Bungeni watagombea upya viti vyao kupitia vyama vyao vipya.