Juhudi za kupoza mitambo Japan

Japan imeongeza jitihada zake za kupunguza joto katika mtambo wa nyuklia huko Fukushima Daiichi, Japan.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Helikopta ikichota maji baharini

Helikopta zilikuwa zikivinyunyuzia maji vyuma katika mtambo huo kuvizuia kuyeyuka.

Wakati hali ya hatari ikiendelea kutishia mitambo ya nyuklia ya kuzalisha umeme huko Fukushima nchini Japan, China imeisihi nchi hiyo jirani itoe maelezo ya haraka na sahihi kuhusu janga hilo la nyuklia.

Tukio hili limepelekea China kusitisha mipango yake ya kuunda mitambo ya nyuklia.

Polisi walisema watu 5400 wamefariki dunia na wengine 9500 bado hawajulikani walipo.