Mabomu mji wa Benghazi, Libya

Jeshi la Libya limetekeleza shambulio lake la kwanza kwa mabomu dhidi ya mji wa Benghazi ambao umekuwa ukidhibitiwa na waasi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waasi Libya

Waandishi wa habari wa BBC walisema walisikia ndege ndogo ikipita pamoja na miripuko kweny mipaka ya mji huo ambao una wakaazi wapatao milioni moja.

Taarifa zinasema kuwa miji ilyokuwa inalengwa ni pamoja na ule wa Benina.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Alhamisi kupiga kura ya kuamua hatua ya kuchukua dhidi ya Libya.

Katika habari zaidi, televisheni ya taifa ya serikali ya Libya inaripoti kuwa majeshi ya Kanali Gaddafi yamechukua udhibiti wa ngome ya waasi, magharibi mwa nchi katika eneo la Misrata, na inawakurupusha waasi huko.

Ingawaje, wakaazi wa Misrata wamedai kuwa waasi bado wanashikilia mji huo.