Chelsea na Man U kukutana kombe la Ulaya

Droo iliyofanywa muda mfupi uliopita imeziweka Chelsea na Manchester United njia panda ambapo vilabu hivyo vitachuana kutafuta nafasi ya kushiriki nusu fainali.

Duru ya kwanza ya mpambano huo utafanyika kwenye uwanja wa Stamford bridge na ya pili kwenye uwanja wa Old Trafford ambapo Manchester United itaridhia kulipiza kisasi endapo mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao katika pambano la kwanza.

Huu ni mfano wa marudio ya fainali ya mwaka 2008 Manchester United ilipoichapa Chelsea kupitia mikwaju ya penati mjini Moscow.

Image caption Ancelloti

Chelsea haijawahi kushinda Kombe la Ligi ya mabingwa na klabu hiyo inajitahidi kufanya vyema katika michuano hiyo ikiwa hali yake kwenye msimamo wa Ligi ya Premiership ni mbaya kiasi kuhitaji ushindi barani Ulaya ili msimu ujao isikose kushiriki michuano ya barani Ulaya.

Droo hiyo pia imeweka uwezekano wa mahasimu wa Ligi ya Uhispania kukutana kwenye hatua itakayofuata robo fainali. Barcelona itapambana na Shaktar Donetsk huku Real Madrid itachuana na Tottenham hotspurs.

Tottenham ambayo imekuwa kivutio cha mashindano haya kwa kuvibwaga vilabu vyenye uzoefu zaidi katika mashindano haya inaingia hatua ya robo fainali kwa nguvu kuwa Real Madrid haijawahi kushinda mbele ya klabu yoyote kutoka England.

Pamoja na hilo Real haijavuka hatua ya robo tangu mwaka 2002. Lakini safari hii ina kocha anayefahamu soka ya England, Jose Mourinho aliyeondoa rekodi ya vilabu vya Ufaransa kuiondoa Real Madrid katika mashindano haya kwa kipindi kirefu.

Endapo vilabu vya Uhispania vitavuka hatua hii basi vitapambana mara nne katika kipindi cha majuma matatu.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Real imepangiwa kukutana na Barcelona katika mchuano wa La Liga tarehe 17 kisha fainali ya Kombe la Mfalme tarehe 20 Aprili mbali na nusu fainali hii ya Ligi ya mabingwa itakayobidi vilabu kucheza nyumbani na ugenini kati ya tarehe 5 na 6 Aprili na mechi za marudiano tarehe 12 au 13 mwezi huo huo. Bingwa mtetezi wa Kombe hili Inter Milan atakwaruzana na Schalke 04, akitazamiwa kuvuka bila matatizo kufuatia jinsi alivyorahisisha safari yake kwa kuichapa Bayern Munich.

Kikamilifu hivi ndviyo ratiba ilivyo. Robo fainali (Aprili 5/6 na Aprili 12/13) Real Madrid (UHISPANIA) v Tottenham Hotspur (ENG) Barcelona (UHISPANIA) v Shakhtar Donetsk (UKR) Chelsea (ENG) v Manchester United (ENG) Inter Milan (ITA) v Schalke 04 (GER) Nusu fainali (April 26-27 na May 3-4) Inter Milan au Schalke 04 v Chelsea au Manchester United Real Madrid au Tottenham v FC Barcelona au Shakhtar Dontesk