Mataifa yajadili hatua dhidi ya Libya

Mataifa yaliyoahidi kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa, linalokataza ndege kuruka katika anga ya Libya, yanakutana mjini Paris, kujadili hatua ya kuchukua.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ndege za kivita za Mataifa ya Magharibi

Viongozi wa Ufaransa, Ungereza na Marekani, wamejumuika na nchi za Jumuiya ya Kiarabu, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon.

Huku ndege za kijeshi zinapelekwa eneo la Mediterranean, Kanali Gaddafi, ameonya Mataifa ya Magharibi, yatajuta, endapo yataingilia kati.

Taarifa yake imesema, azimio la Umoja wa Mataifa, linatoa idhini ya kuingilia kati kijeshi, sio halali.

Mwakilishi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, amesema, anatarajia hatua za kijeshi, zitaanza katika saa chache baada ya mkutano huo wa Paris.