Maandamano nchini Syria, watatu wauawa

Kwa uchache waandamanaji watu wameuwawa nchini Syria wakati wa mapambano dhidi ya vikosi vya usalama katika mji wa Deraa kusini mwa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamaji Syria

Watu wengine kadhaa walijeruhiwa.

Walioshuhudia matukio hayo walisema polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wanadai uhuru zaidi, kumailizika kwa ufisadi na kuvunjwa kwa vikosi vya usalama.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema vikosi vya usalama villingilia kati kuzima vitendo vya ghasia na uharibifu.

Marekani ililaani mauaji hayo na kusema waliohusika na vitendo hivyo wanapaswa kuwajibika.