Gaddafi aahidi vita vya muda mrefu

Kanali Muammar Gaddafi amesema Libya itapigana "vita vya muda mrefu" baada ya nchi za Magharibi kushambulia majeshi yake kwa ndege kulinda maeneo yanayoshikiliwa na waasi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege ya kijeshi ikifyatua bomu kwenda Libya

Maafisa wa kijeshi inaarifiwa wanafanya tathmini ya hasara iliyopatikana baada ya mambomu 110 kuangushwa na Marekani na Uingereza.

Baada ya shambulio moja, miili ya watu 14 ilikuwa imezagaa karibi na gari la kijeshi lililoteketezwa nje ya mji unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi, kufuatia mashambulio yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Ufaransa, limeripoti shirik la habari la Reuters.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikielekea Libya

Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa limeruhusu matumizi ya nguvu kulinda raia.

Mabomu ya kurusha kwa ndege yalilipua vituo visivyopungua 20 vya anga mjini Tripoli, na pia katika jiji la mashariki la Misrata, wamesema maafisa wa kijeshi wa upande wa magharibi.

Televisheni ya taifa ya Libya imeonesha picha za watu 150 waliojeruhiwa katika mashambulio hayo. Imesema watu 48 wameuawa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Shambulio la anga Tripoli

Hakukuwa na taarifa rasmi kuhusu vifo hivyo na waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameiambia BBC kuwa madai hayo yatazamwe kwa makini, kwa sababu wanajeshi wanajitahidi kuepusha vifo vya raia.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya ulinzi Jonathan Marcus anasema wanaoapnga mipango ya kibita wa majeshi ya umoja, watakuwa wakitazama picha za satelaiti kuona hasara waliyosababisha kwa majeshi ya anga ya Kanali gaddafi na pia kuona kama wanahitaji kufanya mashambulio zaidi.

Image caption Hali tete Libya

Amesema pia watakuwa wakifuatilia kwa karibu shughuli za majeshi ya serikali yaliyopo karibu na miji yenye watu wengi, kama vile Benghazi na Misrata, kuona kama wanataka kushambulia ili wazuie.

Mkazi mmoja wa Misrata ameiambia BBC kuwa majeshi yanayomuunga KanaliGaddafi yameanza mashambulio mapya siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Muammar Gaddafi

"Tunawaahidi vita vya muda mrefu, vita visivyo na mwisho," amesema Kanali Gaddafi kwa njia ya simu akizungumza na televisheni ya taifa siku ya Jumapili asubuhi.

Amesema majeshi ya Magharibi hayana haki ya kuishambulia Libya, ambayo haijawafanya lolote.

"Tutapigana sentimita kwa sentimima," amesema, huku picha ya ngumi ya dhahabu ikigonga ndege ya Marekani ikioneshwa.

Awali, alisema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya watu kuilinda Libya na kuelezea mashambulio hayo kama "vita viovu".

Saa za alfajiri siku ya Jumapili, milipuko ya mabomu ilitanda katika anga ya Tripoli na milipuko mingine kadhaa kusikika.