Ndege ya mizigo yapata ajali Congo

Image caption Congo-Brazzaville

Ndege ya mizigo imeanguka katika eneo waishio watu Congo-Brazzaville, kwenye mji mkuu, Pointe-Noire.

Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema aliona gari lililokuwa limebeba miili ya watu waliokufa na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti na waliojeruhiwa kufikishwa hospitali.

Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga Michel Ambende alisema ndege hiyo ilipata ajali wakati ilipotua lakini hakuthibitisha kufariki dunia kwa yeyote.

Kulingana na shirika la habari la AFP, "Kuna uharibifu mkubwa lakini hatuzungumzii waliokufa bado."