Wapiganaji wanaikomboa Ajdabya

Wapiganaji wa Libya Haki miliki ya picha Other
Image caption Wapiganaji wa Libya

Wapiganaji wa mashariki mwa Libya, wameuteka tena mji muhimu wa Ajdabiya, kutoka kwa majeshi ya Muammar Gaddafi.

Ndiyo mji wa kwanza kukombolewa na wapiganaji, tangu kuanza shughuli za kuzuwia ndege za serikali kuruka katika anga ya Libya.

Waziri mmoja wa serikali, Khaled Kaim, alisema jeshi la serikali liliondoka Ajdabiya, baada ya kupigwa kwa mabomu na ndege za jeshi la kimataifa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Libya

Mwandishi wa BBC mjini humo, anasema wapiganaji walicheza mabara-barani, kusherehekea.

Piya anasema, aliona vifaru kama 20 vya serikali, magari ya deraya na mizinga, ambayo iliharibiwa au kuachwa.

Na mashambulio ya ndege, yalitikisa kitongoje kimoja cha mji mkuu, Tripoli, leo alfajiri.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema, mtambo wa jeshi wa radar uliwaka moto.