Wakimbizi kutoka Afrika Kaskazini

Wakuu wa Utaliana wana kazi kubwa ya kushughulikia wakimbizi wanaowasili nchi humo kutoka Afrika Kaskazini.

Wakimbizi kama 300, wengi kutoka Ethiopia na Eritria, wamewasili leo kwa mashua wakitokea Libya, akiwamo mwanamke mmoja na mwanawe mchanga, aliyemzaa kwenye mashua.

Mashua nyengine kadha, zenye mamia ya wakimbizi zinatarajiwa kuwasili Utaliana, katika saa zijazo.

Hadi sasa, Utaliana imepokea watu kama elfu 15 waliokimbia Afrika Kaskazini katika majuma ya karibuni, na imeomba msaada wa kimataifa.