Huwezi kusikiliza tena

Serikali ya Tanzania yatoa ufafanuzi

Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu tiba inayotolewa na mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile anayedai kutibu magonjwa sugu Loliondo kaskazini mwa nchi hiyo huku ikisisitiza kwamba haitaisitisha huduma ya mchungaji huyo.

Badala yake imesema itamsaidia kuboresha mazingira ya kutolea tiba pamoja na kuboresha miundo mbinu ya eneo hilo.

Tangazo hilo la serikali linakuja wakati idadi ya watu wanaokwenda kupata huduma ya dawa kwa mchungaji huyo ikiwa inazidi kuongezeka na wengine kufariki dunia kabla na baada ya kupata dawa hiyo.

Kutoka Dar es Salaam Mwandishi wetu John Solombi anaeleza zaidi.