Waziri wa Libya ahojiwa Uingereza

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Libya Mousaa Koussa

Waziri wa mambo ya nje wa Libya Mousaa Koussa amekuwa akihojiwa na maafisa baada ya kuwasili Uingereza bila kutarajiwa siku ya Jumatano.

Alitokea Tunisia. Ofisi ya Uingereza ya mambo ya nje ilisema "hakuwa na nia tena" ya kufanya kazi na Kanali Gaddafi.

Hata hivyo msemaji wa Libya alikana kwamba Bw Koussa ameasi na kwamba alikuwa katika safari ya kidiplomasia.

Kuwasili kwake Uingereza kumefanyika huku waasi wa Libya wakiwa wamerudi nyuma kwenye miji iliyotekwa hivi karibuni katika pwani ya mashariki.

Kurudi nyuma kwa waasi kulitokana na mapigano makali baina ya Brega na Ajdabiya siku ya Alhamis.

Awali waasi hao walishapoteza bandari muhimu ya mafuta ya Ras Lanuf na mji mwengine ulio karibu wa Bin Jawad.

Upande wa magharibi, mji ulioshikiliwa na waasi wa Misrata bado unaripotiwa kushambuliwa na majeshi ya wanaomtii Kanali Gaddafi.